Timu yafanya mazoezi ya mwisho KMC Complex

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa KMC Complex tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu.

Jambo jema ni kwamba mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons hatujapata mchezaji aliyeumia hivyo kocha Mkuu Fadlu Davids atakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

Kila mchezo ulio mbele yetu tunaupa umuhimu mkubwa lengo likiwa kuibuka na ushindi na kupata pointi tatu.

Tayari kocha Msaidizi Darian Wilken ameweka wazi wakati akiongea na Vyombo vya Habari kuwa utakuwa mgumu ingawa Simba ni kubwa zaidi ya Namungo na tupo kamili kupigania alama tatu.

“Utakuwa mchezo mgumu, Namungo ni timu imara yenye wachezaji wazoefu na tayari imepata kocha mpya, lakini Simba ni kubwa zaidi na ipo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajili ya kupata pointi tatu,” amesema Kocha Wilken.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER