Kauli ya Kocha Wilken kuelekea mchezo dhidi ya Namungo

Kocha Msaidizi, Darian Wilken amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi kwenye uwanja wa nyumbani.

Kocha Wilken amesema Namungo ni timu nzuri hasa ikichangiwa na kuwa na Kocha mpya ambaye amewaongezea morali wachezaji wake lakini itakutana na wapinzani bora zaidi yako.

Wilken ameongeza kuwa pamoja na ugumu wa ratiba wa kucheza mechi karibu karibu kunakosababisha wachezaji kupata majeraha lakini Simba ni timu kubwa na inatakiwa kupambana katika kila mchezo ili kupata pointi tatu.

“Utakuwa mchezo mgumu, Namungo ni timu imara yenye wachezaji wazoefu na tayari imepata kocha mpya, lakini Simba ni kubwa zaidi na ipo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajili ya kupata pointi tatu,” amesema Kocha Wilken.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema kwa upande wao wapo tayari kupambana hadi mwisho kwa ajili ya kupata pointi tatu.

Ally amesema Namungo ina wachezaji wengi wazoefu ambao wengi walikuwa nao lakini Simba ni kubwa na pamoja na changamoto zote ila tupo tayari kwa ajili ya pointi tatu muhimu za nyumbani.

“Sisi tupo tayari kwa mchezo, Namungo tunawaheshimu ni timu bora lakini Simba ni bora zaidi na tupo kwa ajili ya kupigania alama tatu,” amesema Ally Salim.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER