Tumepata pointi tatu muhimu Sokoine

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mlinzi wa kati Che Fondoh Malone alitupatia bao la kwanza dakika ya tano kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Kibu Denis kumponyoka mlinda mlango Mussa Mbisa.

Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Prisons huku tukifanya mashambulizi mengi lakini kikwazo kilikuwa mlinda mlango Mbisa.

Kipindi cha pili tulirejea kwa kasi huku tukiliandama lango la Prisons lakini hata hivyo tulipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi 16 tukiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi saba.

X1: Mbisa, Mbangula, Mwasilindi, Haji, Shaban, Mpesa, Mayombya, Chanongo (El Fadhili 67′), Mwihambi, Jeremia (Ismail 67′), Sadoki

Walioonyeshwa kadi: Haji Mussa 27′ Dotto 74′

X1: Camara, Kapombe Zimbwe Jr (Balua 62′)Che Malone, Chamou, Ngoma, Kibu, Okajepha, Ateba (Mukwala 72′)*, Awesu (Mutale 62′), Chasambi (Mzamiru 84′)

Walioonyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER