Tupo tayari kuikabili Prisons Sokoine Leo

Kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa saa 10 jioni.

Ni mchezo muhimu kupata alama tatu hasa ukizingatia hatujapata matokeo mazuri kwenye mechi mbili za ligi zilizopita.

Utakuwa mchezo mgumu hasa kwakuwa tunacheza ugenini lakini tupo tayari kuhakikisha tunapambana hadi mwisho ili kupata ushindi.

Fadlu azungumzia ugumu wa ratiba…

Kocha Mkuu Fadlu Davids ameweka wazi kuwa hatujapata muda wa kufanya hata mazoezi hasa ukizingatia tumetoka kucheza mechi ngumu ya Dabi mwishoni mwa juma.

Fadlu ameongeza kuwa ratiba ni ngumu na wachezaji hawapati muda wa kupumzika lakini tutapambana kuhakikisha tunashinda.

“Itakuwa mechi ngumu, tunacheza katika Uwanja ambao sio rafiki sana na pia tumetoka kucheza mechi ngumu huku tukiwa hatujapata muda mzuri wa kufanya mazoezi,” amesema Kocha Fadlu.

Zimbwe Jr awatoa hofu Wanasimba

Nahodha wa timu Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amewaomba Wanasimba kutokatishwa tamaa na matokeo ya mechi mbili bali waendelee kuisapoti timu ili kuweza kupata ushindi.

Zimbwe amesema hata wachezaji wanaumia kunapokosekana ushindi lakini kwenye kila mechi wanapambana ili kuwapa furaha mashabiki.

“Tunazidi kuwaomba mashabiki wetu kuendelea kutupa sapoti, msikatatishwe tamaa na matokeo ya mechi mbili zilizopita, sisi wachezaji wenu tunapambana ili kuwapa furaha,” amesema Zimbwe Jr.

Hali ya kikosi……

Kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri na tumesafiri na wachezaji 22 ambao wote wamefanya mazoezi ya mwisho jana na wapo fiti kwa mchezo wa leo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER