Simba Queens imeanza na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Mlandizi Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) uliopigwa Uwanja wa TFF Center Kigamboni.
Mchezo huo ulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la Mlandizi lakini walinzi wao walikuwa imara kuhakikisha hawaruhusu bao la mapema.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo dakika ya 52 Asha Rashid ‘Mwalala’ alitupatia bao la kwanza baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Elizabeth Wambui.
Dakika ya 58 Mwalala alitupatia bao la pili baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Mlandizi.
Asha Djafar alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la tatu dakika ya 75 baada Ya kuunganisha pasi ya kichwa ya Esther Mayala.
Kocha Yassif Basigi alifanya mabadiliko ya kumtoa Mwalala na kumuingiza Jentrix Shikangwa.