Mchezo wa tano wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union uliopigwa Uwanja wa KMC Complex umemalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Tulianza mechi hiyo ilianza kwa kasi huku tukifanya mashambulizi mengi langoni mwa Coastal katika dakika 15 za mwanzo lakini walikuwa imara kuondoa hatari.
Nahodha Mohamed Hussein alitupatia bao la kwanza dakika ya 25 baada ya mpira uliopigwa na Joshua Mutale kumponyoka mlinda mlango Ley Matampi.
Mshambuliaji Leonel Ateba alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Mlinzi mmoja wa Coastal Union kuunawa mpira ndani ya 18.
Kipindi cha pili Coastal walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la gnm dakika ya 48 baada ya Abdallah Hassan kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango Moussa Camara.
Hernest Malonga aliwapatia Coastal bao la kusawazisha dakika ya 72 kufuatia mlinda mlango Camara kutoka nje ya lango bila kuchukua tahadhari.
Kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko ya kuwatoa Joshua Mutale, Deborah Fernandez na Kibu Denis na kuwaingiza Awesu Awesu, Fabrice Ngoma na Kibu Denis.