Mgosi: Tupo tayari kutetea Ngao ya Jamii

Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi amesema wachezaji wapo tayari ajili ya kutetea taji lao la Ngao ya Jamii kwa kucheza dhidi ya mpinzani wake Yanga Princess.

Mgosi amesema Yanga Princess wamefanya usajili mzuri na wanatamani kuwa kama Simba na hawahitaji kuwa kama wapinzani wetu kwa sababu tupo mbali tumecheza mechi nyingi za kiushindani.

Mgosi amesema hayo katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Princess utakaochezwa kesho uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge Dar es Salaam.

“Tumefanya maandalizi mazuri, tuko vizuri lakini tutacheza kwa tahadhari kubwa kwa sababu Yanga Princess wamefanya usajili mzuri na wamemrejesha kocha Edna Lema ambaye ni mzoefu wa soka la Wanawake,” amesema Mgosi.

Kwa niaba ya wachezaji mlinzi Fatma Issa ‘Fetty Densa’ amesema wamejipanga vizuri kazi imebaki kwa wachezaji na hawatawaangusha mashabiki wao kupambana kutetea taji hilo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER