Timu yakutana na Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi

Viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wamepata nafasi ya kukutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi leo mchana baada ya kuwasili visiwani Zanzibar.

Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu Zanzibar tumemkabidhi zawadi ya jezi Rais Dkt. Mwinyi pamoja na mke wake mama Mariam Mwinyi.

Akizungumzia katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Rais Dkt. Mwinyi ametupongeza kwa namna tunavyoiwakilisha nchi kimataifa kwani jambo hilo linasaidia kukuza utalii kupitia michezo.

Pia Rais Dkt. Mwinyi amesema serikali yake imejipanga kuendelea kuboresha na kujenga viwanja vya michezo ambavyo vitakuwa na vigezo vya kutumika kwenye michuano ya AFCON 2027 na CHAN 2025 hivyo kutukaribisha muda wowote kuja Zanzibar kuchezea michezo ya mashindano ya ndani na kimataifa.

“Niwapongeze wachezaji, benchi la ufundi na Viongozi kwa kuipeperusha vema bendera ya nchi Kimataifa, Serikali tunajivujia nyinyi na mara zote tupo nyuma yenu.”

“Sisi kama Serikali tutaendelea kuboresha miundombinu ya michezo, na nichukue nafasi hii kuwakaribisha Zanzibar kuja kucheza mechi zenu iwe kitaifa au Kimataifa,” amesema Rais Mwinyi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo lakini pia ametumia nafasi hiyo kuwasilisha ombi la Simba kupata eneo ambalo tutajenga kituo cha kukuzia vipaji vya mpira wa miguu (Academy) Visiwani humo.

“Muheshimiwa Rais unafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwa wanachi nasi tunaithamini lakini pia naomba kuwasilisha ombi letu la kuhitaji eneo kwa ajili ya kujenga Kituo cha kukuza vipaji,” amesema Mangungu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER