Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Al Hilal kutoka Sudan katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa.
Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji sita ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC.
Kocha Fadlu amewaanzisha Aishi Manula, Valentine Nouma, Karaboue Chamou, Kibu Denis, Lionel Ateba na Ladaki Chasambi kuchukua nafasi ya Moussa Camara, Mohamed Hussein, Abdulrazack Hamza, Mzamiru Yassin Edwin Balua, Steven Mukwala na Jean Charles Ahoua.
Hiki hapa kikosi kamili kilivyopangwa:
Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Valentine Nouma, Che Malone (20), Karaboue Chamou (2), Yusuph Kagoma (21), Kibu Denis (38), Debora Fernandes (17), Lionel Ateba (13), Ladaki Chasambi (36), Awesu Awesu (23).
Wachezaji wa Akiba
Hussein Abel (30), David Kameta (3), Hussein Kazi (4), Kelvin Kijili (33), Abdulrazack Hamza (14), Mzamiru Yassin (19), Omary Omary (8), Augustine Okajepha (25), Joshua Mutale (7), Saleh Karabaka (16), Valentino Mashaka (27).