Mchezo wetu wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Kawempe Muslim kutoka Uganda.
Kawempe walipata bao la mapema dakika ya 10 kupitia kwa Sumayah Nabuto baada ya kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango Gelwa Yonah.
Baada ya bao hilo tuliendelea kuliandama lango la Kawempe ili kupata bao la kusawazisha lakini walikuwa makini kuzuia mashambulizi.
Agnes Nabukenya aliwapatia Kawempe bao la pili dakika ya 50 baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni.
Kocha Mkuu Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Asha Rashid, Jackine Albert, Amina Bilali na Esther Mayala na kuwatoa Jentrix Shikanga, Wincate Kari, Asha Djafari na Mary Saiki.
Mchezo wa leo umehitimisha safari yetu ya michuano hii katika msimu huu wa mashindano mwaka 2024.