Leo saa tano asubuhi kikosi chetu cha Simba Queens kitashuka katika Uwanja wa Abebe Bikila kuikabili Kawempe Muslim kutoka Uganda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kocha Juma Mgunda amefanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi ya mwisho dhidi ya Polisi Bullets kutoka Kenya.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Gelwa Yonah (21), Fatuma Issa (5), Wincate Kaari (12), Ruth Ingosi (20), Violeth Nicholaus (26), Mary Saiki (19), Elizabeth Wambui (4), Ritticia Nabbosa (13), Jentrix Shikangwa (25), Vivian Corazone (17), Asha Djafar (24).
Wachezaji wa Akiba:
Janeth Shija (1), Esther Mayala (23), Daniela Ngoyi (22), Jackline Albert (16), Amina Bilali (11), Precious Christopher (8), Asha Mwalala (14), Shelda Boniface (9).