Simba Queens imefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Abebe Bikila kwa ajili ya mchezo wa kesho wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Kawempe Muslim kutoka Uganda.
Nahodha wa timu, Violeth Nicholas amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho ili kupata nafasi ya tatu.
Violeth amesema malengo yetu yalikuwa kuingia fainali na baadae kutwaa ubingwa lakini kwakuwa imeshindikana kilichobaki ni kupigania kilichopo mbele yetu.
“Tupo tayari kwa mchezo, tunajua itakuwa mechi ngumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tupo tayari.”
“Tumeumia kwa kushindwa kuingia fainali lakini tunajua huu ni mpira na sasa tunaangalia kilichopo mbele yetu,” amesema Violeth.
Kawempe tulikuwa nao kundi moja na katika mchezo wa hatua ya makundi tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.