Tumefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.
Edwin Balua alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 13 baada ya kumalizia mpira krosi uliopigwa na Jean Charles Ahoua.
Steven Mukwala alitupatia bao la pili dakika ya 44 baada ya kumalizia pasi safi kutoka Shomari Kapombe.
Jean Ahoua alitupatia bao la tatu dakika ya 59 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka Balua.
Valentino Mashaka alitupatia bao la nne dakika ya 81 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Ahoua.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi sita baada ya kucheza mechi mbili tukifunga mabao saba huku tukiwa hatujaruhusu bao lolote.
X1: Camara, Kapombe (Kijili 65′), Zimbwe Jr, Hamza, Che Malone, Mzamiru (Kagoma 55′), Balua (Karabaka 81′), Fernandes, Mukwala (Mashaka 55′), Ahoua, Awesu (Kibu 65′).
Walioonyeshwa kadi:
X1: Fikirini, Lulambo Kadikilo, Hebrone, Makame, Kulandana, Ambundo (Mwampangama 48′), Kassim, Kilemile (Zamfuko 83′), Sadick (Mwalimu 48′), Kihimbwa
Walioonyeshwa kadi: Laurian Makame 74′ Erick Nkosi 86′