Timu yafanya mazoezi ya mwisho KMC Complex

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa KMC Complex kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC utakaopigwa kesho saa 10 jioni.

Wachezaji wote isipokuwa Joshua Mutale na Ayoub Lakred ambao ni majeruhi wameshiriki mazoezi hayo na wapo tayari kwa mchezo wa kesho.

Katika mazoezi hayo yaliyoongozwa na Kocha Mkuu Fadlu Davids na wasaidizi wake hakuna mchezaji aliyepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya kuukosa mchezo wa kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER