Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanya mazoezi ya utimamu wa mwili asubuhi katika Uwanja wa TESFA MEDA baada ya ushindi mabao 5-0 tulipata jana dhidi ya FAD Djibouti.
Mazoezi ya utimamu ni muhimu kiafya kwa wachezaji kwakuwa yana urejesha mwili katika hali ya kawaida baada kutumia nguvu nyingi kwa wakati mmoja.
Simba Queens itashuka tena dimbani kesho Jumatano saa tano asubuhi kuikabili Kawempe Muslim ya Uganda katika mchezo wa pili wa kundi B.
Kawempe Muslim waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya RVP Buyenzi katika mchezo wa kwanza.