Mchezo wetu wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) dhidi ya FAD Djibouti uliokuwa upigwe kesho sasa utafanyika Jumatatu.
Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu nane kutoka kwenye makundi mawili inaanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa Abebe Bikila nchini Ethiopia.
Mabadiliko haya ya ratiba yanakipa nafasi kikosi chetu kuendelea kuzoea hali ya hewa ya Ethiopia ambayo ni baridi.
Morali za wachezaji zipo juu na wanaendelea na programu za mazoezi chini ya Kocha Juma Mgunda na wasaidizi wake