Mshambuliaji Leonel Ateba amejiunga na kikosi chetu kutoka USM Alger ya Algeria kwa mkataba wa miaka miwili.
Ateba ambaye ana umri wa miaka 25 raia wa Cameroon amewasili nchini leo na tayari amefanyiwa vipimo vya Afya na amefuzu.
Usajili wa Ateba ni pendekezo la kocha Fadlu Davids ambaye ametaka kuimarisha safu yetu ya ushambuliaji kuelekea msimu huu wa mashindano.
Ateba analijua vizuri soka la Afrika na amewahi kuzichea timu mbalimbali kama PWD Bamenda, Dynamo Douala ya Cameroon na USM Alger na pia kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon ‘Indomitable Lions’.
Tayari amejiunga na wenzake kuendelea na maandalizi ya mchezo wetu wa kwanza wa Ligi dhidi ya Tabora United.