Simba Queens yapokelewa vizuri Ethiopia

Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia umeipokea timu yetu ya Simba Queens ambayo imewasili kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mwakilishi wa Balozi nchini hapa, Brigedia Jenerali Mohamed Suleiman amesema ingawa tumeenda kama klabu lakini tunahesabika kama taifa kutoka Tanzania na tutapata kila ambacho tunastahili.

Brigedia Jenerali Mohamed amesema kwa kukiona kikosi chetu amepata matumaini makubwa kuwa tutafanya vizuri kwenye michuano hii.

Aidha Brigedia Jenerali Mohamed ameongeza kuwa tunatakiwa kuhakikisha tunafanya vizuri kuanzia mchezo wa kwanza hadi wa mwisho ambao tutakabidhiwa taji na kurudi nalo Tanzania.

“Karibuni sana nchini Ethiopia. Ubalozi wa Tanzania utakuwa pamoja nanyi kwa siku zote mtakazokuwa hapa na mtapata kila mnachostahili.”

“Balozi wetu alipenda awepo mwenyewe kuja kuwapokea lakini yupo nje ya nchi na ametutuma sisi kuja kumuwakilisha. Kwa kuwatazama machoni nina imani kubwa ya kikosi hiki na tutafanikiwa kuchukua ubingwa,” amesema Brigedia Jenerali Mohamed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER