Tumepoteza mchezo wa Ngao ya Jamii

Mchezo wetu wa Ngao ya Jamii umemalizika kwa kupoteza kwa bao moja dhidi ya watani wetu Yanga mtanange uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini kulikosekana umakini wa kutumia nafasi chache zilizotengenezwa katika dakika 30 za mwanzo.

Maxi Nzengeli aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 43 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi ya Prince Dube.

Kipindi tulirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Yanga na kutengeneza nafasi lakini hata hata hivyo hatukuweza kuzitumia.

Pamoja na mashambulizi ya pande zote lakini hata hivyo hakuna kilichoweza kubadili matokeo.

Matokeo haya yanatufanya kukutana na Coastal Union katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa saa tisa alasiri.

X1: Camara, Kapombe (Kijili 78′), Zimbwe Jr, Che Malone, Chamou, Mzamiru (Okajepha 45′), Balua (Freddy 79′), Fernandes (Ngoma 70′), Mukwala (Kibu 70′), Ahoua, Mutale

Wakionyeshwa kadi: Chamou 78′

X1: Diarra, Yao, Boka, Bacca, Job, Aucho, Abuya (Mudathir 66′), Nzengeli (Mwamnyeto 87′), Dube ( Mzize45′), Aziz Ki (Chama 81′), Pacome (Musonda 87′)

Wakionyeshwa kadi: Aucho 37′ Pacome 84′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER