Tupo tayari kwa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii

Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuikabili Yanga kwenye mchezo wa Nusu Fainali Ngao ya Jamii.

Kikosi kipo kwenye hali nzuri na wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho jana Uwanja wa Mo Simba Arena na wapo kwenye hali nzuri.

Tunafahamu ni mchezo muhimu na mgumu lakini tunahitaji kushinda ili kutuongezea morali kuelekea msimu ujao wa Ligi.

Kocha Fadlu afunguka…..

Pamoja na ubora walionao wapinzani wetu lakini tutaingia kwenye mchezo wa leo bila kuwa na presha.

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema tuna kikosi imara ambacho tuna wachezaji bora kila nafasi hivyo tupo tayari kuikabili Yanga na kupata ushindi.

“Mchezo wa leo utatupa mwanga kuelekea msimu ujao wa Ligi, utatuonyesha maandalizi yetu ya wiki tatu kule Misri yalikuwaje.

“Hatuna presha tutaingia kwenye mchezo wa leo kama ilivyo kwenye mechi nyingine lakini tumejipanga tunapata ushindi,” amesema Kocha Fadlu.

Zimbwe Jr aongea kwa niaba ya wachezaji..

Nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na watafanyia kazi maagizo watayopewa na walimu.

“Maandalizi yetu yamekamilika, sisi kama wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na walimu wetu lakini lengo letu ni kushinda,” amesema Zimbwe Jr.

Nyota 14 wanacheza Derby ya kwanza

Wachezaji 14 ambao tumewasajili katika dirisha hili la usajili leo watakuwa wanacheza mechi ya kwanza ya Derby dhidi ya watani Yanga.

Wachezaji hao ni Moussa Camara, Kelvin Kijili, Valentine Nouma, Karaboue Chamou, Abdulrazack Hamza, Augustine Okajepha, Yusuph Kagoma, Debora Fernandes, Joshua Mutale, Jean Charles Ahoua, Omary Omary, Awesu Awesu, Steven Mukwala na Valentino Mashaka.

Sisi ndio Mabingwa Watetezi wa Ngao

Agosti 14 mwaka jana tuliitwaa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati katika mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER