Leo tutacheza mechi ya pili ya kirafiki Misri

Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Mercure kuikabili Telecom FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri.

Mchezo huu ni wa pili wa kirafiki baada ya ule tuliocheza dhidi ya Al Qanah ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Tulivyomaliza wiki ya kwanza ya mazoezi tulivyofika nchini Misri tulicheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe ambapo wachezaji wetu waligawanywa kwenye makundi mawili.

Mchezo wa leo utaendelea kumpa nafasi kocha Fadlu Davids na wasaidizi wake kuona wachezaji wameyashika mafunzo kwa kiasi gani.

Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Telecom na tunaamini kitakuwa kipimo kizuri kwetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER