Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally ametunukiwa tuzo ya matumizi fasaha ya Lugha ya Kiswahili na Taasisi ya Watetezi wa Kiswahili Tanzania (WAKITA).
Tuzo hiyo amekabidhiwa na Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Maadhimisho ya miaka 10 ya WAKITA yaliyofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ahmed amekabidhiwa tuzo hiyo kutokana na weledi wake wa kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.