CEO Kajula aongoza safari ya Moro

Mtendaji Mkuu, Imani Kajula amewaongoza Wansimba kwenye safari ya kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya uzinduzi wa Wiki ya Simba.

CEO Kajula ameongozana na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Viongozi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Uzinduzi wa Wiki ya Simba umefanyika katika Stendi ya Mabasi Morogoro ambapo Wanasimba kutokana maeneo mbalimbali ndani ya nje ya mkoa huo wamehudhuria.

Kikosi cha hamasa kikiongozwa na Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally nacho kilikuwepo kwa ajili ya kuwapa furaha Wanasimba kuanzia Kituo cha Treni ya Mwendokasi (SGR) hadi Morogoro.

Baada ya uzinduzi wa Wiki ya Simba kikosi kitaondoka kuelekea Mbugani Mikumi ambapo huko zoezi la uzinduzi wa jezi zetu kwa ajili ya msimu mpya wa mashindano 2024/25 utafanyika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER