Kikosi chazidi kujifua kuelekea mechi dhidi ya AS Vita

Kwa siku tatu mfululizo kikosi chetu kimeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 3, mwaka huu.

Mazoezi yanafanyika chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomez huku wachezaji kutoka timu ya wakubwa wakiwa tisa pekee wengine wakiwa chini ya umri wa miaka 20.

Kwa mara ya kwanza tumetoa wachezaji 18 kwenda kwenye timu zao za taifa tukiwa tumeandika historia kwani haijawahi kutokea kabla kitu ambacho kimemfanya Kocha Gomez kuhitaji kufanya mazoezi pamoja na timu ya vijana.

Mara tu wachezaji 18 waliopo kwenye majukumu ya timu zao taifa kumaliza watarejea mara moja kujiunga na wenzao na maandalizi ya pamoja yatafanyika kuivaa Vita.

Tutaingia kwenye mchezo huo tukiwa vinara wa kundi A kwa pointi ambapo tunahitaji ppinti moja pekee kujihakikishia kuingia Robo Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa tukisaliwa na mechi mbili.

SHARE :
Facebook
Twitter

7 Responses

  1. maoni yangu kwa wachezaji wa timu yangu ya simba tusiingie na matokeo mkononi kwamba kwa mkapa hatoki mtu cha umuhimu ni kupambana kadri ya uwezo wetu ili tutoke na point 3 muhimu najua kua timu tunayo kutana nayo ningumu ukizingatia nayo inaitaji point 3 pia kwaio inatakiwa tuwe makini sana japo tupo kinara wa kundi ila tukishinda hii mechi ya tarehe 3 itatuweka nafasi nzuri zaid ambayo itatuweka sehemu nzuri sana na uhakika wa kucheza robo fainali ya club bingwa africa NGUVU MOJA KWA WANA SIMBA SC wote na viongozi wetu wote na pongezi kubwa ni kwa MH RAIS WA NCHI YANGU MAMA SAMIA SULUHU HASSANI mwenyezimungu amjalie maisha mema na kumpa nguvu insha allah tuta timiza kauli ya HAYATI DK JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI ya kuja na kombe la CLUB BINGWA AFRICA MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALIPEMA PEPONI AAMIIN

  2. Mungu awawezeshe wachezaji wetu walio ktk majukumu ya timu zao za taifa kurejea mapema na wakiwa salama ili waweze kuwahi mazoezi kwaajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya As vital club.

  3. Mchezo muhimu Sana tunahitaji point 3 ili kujiweka nafasi nzuri ya kucheza robo final na team ambayo tuta I mudu vizuri #Nguvumoja

  4. Pamoja daima ndiyo mafanikio yetu.Tuimarike,tushikamanike,tuunganike kama kauli mbiu yetu isemavyo pamoja umoja wetu ndiyo nguvu ya mafanikio.

  5. Tumuenzi Mhe. Hayati John Pombe Magufuli kwa kuchukua ndoo ya CAFCL, All the best my Champions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER