Mo akutana na Viongozi wa SEN

Rais wa heshima ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji ‘Mo’ amekutana na kufanya mazungumzo na mtandao wa Simba Executive Network (SEN) lengo likiwa kujadiliana mambo mbalimbali ya maendeleo.

SEN ni mtandao wa mashabiki wa Simba ambao huchangia ada ya 1,500,000 kwa mwaka kwa ajili ya miradi maalumu ya miundombinu ya klabu.

Wanachama wa SEN hupata faida nyingi kama bima za maisha, tiketi za mechi na faida nyingine nyingi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa SEN akiwapo Mwenyekiti Abdulrazak Badru, Makamu wake Farouk Baghoza, Katibu Dkt. George Ruhago, Katibu Msaidizi Richard Mwalibwa na wanachama wa SEN.

Menejimenti ya Simba iliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER