Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba na kiungo mkabaji Babacar Sarr.
Babacar alijiunga nasi katika dirisha la usajili la mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na timu ya US Monastir ya Tunisia.
Tulikuwa na matumaini na Babacar kutokana na uwezo mkubwa alionao lakini ameshindwa kuendana na kasi ya timu.
Katika kipindi chote cha miezi sita alichokuwa nasi Babacar amekuwa mchezaji imara na mara zote alipopata nafasi alijitoa kwa asilimia 100 kuhakikisha timu inapata matokeo chanya.
Tunamtakia kheri katika maisha mapya ya soka nje ya Simba siku zote tutaendelea kuthamini mchango wake ndani ya kikosi chetu.