Valentin Nouma ni Mnyama

Mlinzi wa kushoto Valentin Nouma raia wa Burkina Faso amejiunga nasi kutoka klabu ya St. Eloi Lupopo ya DR Congo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Valentin ana umri wa miaka 24 ana uwezo mkubwa wa kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja.

Valentin ni mchezaji bora msimu wa 2022/23 akishinda tuzo ya beki bora wa mwaka katika ligi ya Burkinafaso akichezea klabu ya AS Douanes.

Ubora mwingine aliokuwa nao Valentine ni kufunga kwa kutumia mipira ya adhabu pamoja na uwezo mkubwa wa kufunga mikwaju ya penati.

Kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25 tunaboresha kikosi chetu katika kila idara ili kuwa na wachezaji wenye viwango vya hali ya juu.

Valentine anakuja kuongeza nguvu upande wa kushoto akisaidiana na Mohammed Hussein ambapo msimu uliopita alikua mchezaji pekee anaecheza nafasi hiyo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER