Fadlu Davids ndiye kocha wetu Mkuu

Tumefikia makubaliano ya kumuajiri Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 43 kuwa Kocha wetu Mkuu kwa mkataba wa miaka miwili.

Kabla ya kujiunga nasi msimu uliopita Fadlu alikuwa kocha Msaidizi wa miamba ya soka nchini Morocco Raja Casablanca.

Fadlu ambaye enzi zake alikuwa akicheza katika nafasi ya ushambuliaji anachukua nafasi ya Abdelhak Benchikha ambaye aliondoka wakati msimu wa 2023/24 ukiwa unaelekea ukingoni.

Mara nyingi Fadlu amekuwa muumini wa mfumo wa 4-2-3-1 ambao amekuwa akiutumia katika kila timu anayofundisha.

Fadlu analijua vema soka la Afrika kutokana na kuwahi kuzifundisha timu za Maritzburg United ya Afrika Kusini kwa nyakati tofauti pamoja na Orlando Pirates.

Mbali na kufundisha Afrika pia Fadlu amewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Lokomotive Moscow ya Urusi.

Uongozi wa klabu unaamini uwezo alionao Fadlu utaweza kutufikisha katika malengo tuliyojiwekea.

Fadlu amekuja pamoja na wasaidizi wake wote kama ifuatavyo:

Kocha Msaidizi – Darian Wilken raia wa Afrika Kusini

Kocha wa Makipa – Wayne Sandilands raia wa Afrika Kusini

Kocha wa viungo – Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini

Mchambuzi wa mechi – Mueez Kajee raia wa Afrika Kusini

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER