Kibu D yupo sana Simba

Kiungo mshambuliaji Kibu Denis ataendelea kusalia klabuni baada ya kuongeza mkataba mpya wa miaka miwili.

Kibu ni mmoja wa wachezaji anayejitoa muda wote na mpambanaji uwanjani na anastahili kuwepo kwenye mipango ya timu kuelekea msimu ujao wa Ligi 2024/25.

Mipango ya klabu ni kuhakikisha tunasuka kikosi imara kwa ajili ya mashindano mbalimbali na Kibu ni sehemu ya mpango wa timu.

Kibu ni mchezaji mzawa ambaye amejipambanua mwenyewe kutokana na jitihada kubwa anazofanya akiwa uwanjani kwa ajili ya kuisaidia timu na hilo ndilo linamfanya kuwa kipenzi cha Wanasimba.

Uongozi wa klabu umepanga kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi ili kuhakikisha tunarejesha makali ya kikosi chetu na kuwa na timu imara yenye kupigania mataji.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER