Mlinzi, Israel Patrick Mwenda amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kusalia katika kikosi chetu.
Israel ambaye anamudu kucheza kama mlinzi wa kulia na kushoto alijiunga nasi mwaka Julai, 2021 akitokea KMC.
Israel ni miongoni mwa wachezaji ambao tunaamini katika uwezo wake na katika kujenga timu mpya kuelekea msimu ujao wa 2024/25.
Israel ni mchezaji kijana ambaye bado ana nguvu ya kuitumikia timu na uwezo alionao tuna matarajio makubwa juu yake na ataendelea kusalia kwa miaka mitatu mingine.
Uongozi wa Klabu unaendelea kuwapa mikataba wachezaji ambao tutaendelea nao kwakuwa tunahitaji kusuka upya kikosi.