Timu yetu imefanikiwa kuibuka na ushindi mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Tulianza mchezo huo kwa kasi huku tukitengeneza nafasi lakini dakika 20 za mwanzo tulipoteza umakini.
Freddy Michael alitupatia bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 35 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Saido Ntibazonkiza.
Saleh Karabaka alitupatia bao la pili dakika 65 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Mzamiru Yassin.
X1: Lakred, Israel, Zimbwe Jr (Duchu 70′), Che Malone, Kazi, Mzamiru, Willy Onana (Karabaka 45′), Ngoma (Kanoute 70′), Freddy (Jobe 81′), Ntibazonkiza (Chasambi 45′), Balua
Walioonyeshwa kadi: Mzamiru 68′
X1: Makaka, Kasami, Kazi, Nasry, Luseke, Hilary, Tiote, Bwenzi (Juma 54′), Ilanfya, Nyangi (Karihe 65′), Kapama