Timu kuondoka Alfajiri kuelekea Misri

Msafara wa takribani watu 50 mpaka 60 utaondoka kesho saa 11 alfajiri kuelekea nchini Misri tayari kwa mchezo wa Ijumaa wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Uwanja wa Cairo saa tano usiku.

Katika msafara huo wachezaji watakuwa 23, benchi nzima la ufundi, Wawakilishi kutoka Menejimenti ya klabu pamoja na mashabiki 17.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema msafara utaondoka na Ndege ya Shirika la Ndege la Misri na wataenda moja kwa moja hadi Cairo na kufika kesho saa tano asubuhi.

Ahmed amesema baada ya kikosi kufika Cairo wachezaji watapumzika kwa saa chache na jioni kitaendelea na mazoezi.

“Tunatarajia kuondoka kesho alfajiri kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wetu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa usiku.

“Orodha ya wachezaji 23 ambao tutaondoka nao itatolewa baada ya kukamilika kwa mazoezi ya jioni, na tunaenda tukiwa na matumaini ya kwenda kufanya vizuri,” amesema Ahmed.

Ahmed ameongeza kikosi kilirejea mazoezini siku moja baada ya mchezo wa kwanza na morali za wachezaji zipo juu na wapo tayari kwenda kupambana hadi mwisho na malengo ya kufuzu nusu fainali bado yapo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER