Timu yetu ya Simba Queens imeibuka na ushindi mnono wa mabao 14-0 dhidi ya Kinondoni Queens katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.
Mchezo huo ulikuwa wa upande mmoja huku Queens ikitawala karibia kila idara kuanzia mwanzo wa mchezo hadi mwisho.
Katika mchezo huo mabao yetu yalifungwa na Jentrix Shikangwa, Danai Bhobo, Shelda Boniface na Zainabu Mohamed waliofunga mawili kila mmoja.
Mengine yamefungwa Diakiese Kaluzodi, Silivia Mwacha, Asha Rashid, Asha Djafar, Aisha Mnuka na Olaiya Barakat.
Katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu ya Wanawake imesimama kikosi chetu kinaendelea na mazoezi pamoja na kucheza mechi za kirafiki.