Tunaitaka Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally ameweka wazi mipango ya klabu ni kuhakikisha timu inatinga nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuitoa Al Ahly.

Ahmed ameyasema hayo akiwa Tawi la Wekundu wa Feri wakati wa kuzungumzia mchezo wetu wa robo fainali ya michuano hiyo ambao mechi ya kwanza itapigwa Machi 29 jijini Dar es Salaam wakati ile ya amrudiano ikichezwa, Cairo Aprili 5.

Ahmed amesema katika kipindi cha miaka mitano tumejifunza mambo mengi kwenye michuano hii na sasa umefika muda wa kufuzu licha ya kukutana na timu bora na yenye rekodi nzuri.

Ahmed amekiri kuwa Al Ahly ni timu bora na ina historia kubwa Afrika lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kufuzu nusu fainali na kinachotakiwa kuwa na umoja na ushirikiano.

“Tumejifunza mambo mengi kupitia michuano hii katika miaka hii mitano. Huu ni muda wetu wa kuweka historia ya kutinga nusu fainali tena kwa kumtoa bingwa mara 10 wa michuano hii.

“Kinachotakiwa tunahitaji kuwa na mshikamano na kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji, jambo jema ni kwamba mechi itakuwa usiku na kila mtu atakuwa amefuturu kwahiyo hakuna sababu ya Mwanasimba kuacha kuja Uwanjani,” amesema Ahmed.

Ahmed amevitaja viingilio vya mchezo huo kuwa kama ifuatavyo:

Mzunguko Tsh. 5,000
Machungwa Tsh. 10,000
VIP C – Tsh. 20,000
VIP B – Tsh. 30,000
VIP A – Tsh. 40,000
Platinum – Tsh. 200,000
Tanzanite – Tsh. 250,000

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER