Kwa kushirikiana na Benki ya CRBD leo tumezindua Mtandao Mpya wa Simba Executive Networks ambao lengo lake kubwa ni kukusanya pesa kuendeleza miundombinu ya klabu ukiwemo Uwanja wetu wa Mo Simba Arena.
Mtandao huu utaongozwa na Viongozi waandamizi ambao moja ya kazi zao ni kuhakikisha miradi ya klabu inasimamiwa na kufanyiwa kazi kama kuwekwa taa na majukwaa katika Uwanja wa Mo Simba Arena ili kuweza kutumika kwa mechi za usiku.
Simba Executive Networks itaongozwa na Mwenyekiti wa Abdulaziz Badru huku Mlezi wake akiwa Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mussa Azan Zungu.
Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema ili kuwa mwanachama wa Mtandao huu anatakiwa kulipia kiasi cha Shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) kwa mwaka ambapo atalipa kwa miezi mitatu, sita au mara moja kwa mkupuo.
Miongoni mwa vitu anavyopata mwanachama wa Simba Executive Networks
π Kila mwaka atapata jezi mpya za kila msimu, kupata tiketi za mechi kubwa na kimataifa
π Kupata Bima za maisha
π Kutumia miradi yetu kama Uwanja wetu wa Simba Mo Arena kucheza mechi za mabonanza na kufurahia.
Mwanachama wa Simba Executive Networks ambaye atakuwa na kadi ya CRDB atakuwa na uwezo wa kupata yafuatayo.
π Atapata Premier Lounge kwenye matawi ya CRDB nchini nzima
π Uwanja wa Ndege ukiwa unasubiri Ndege kwa ajili ya safari utakuwa unakula na kunywa.
π Saa 24 utakuwa unapata sapoti kutoka CRDB
π Kupata Huduma ya Rufaa ya Visa ya Kimataifa
π Kununua vitu online popote na kama kikiwa kimeharibika au hakijafika utarejeshewa hela yako
π Mwenye kadi akifariki anapewa milioni tano, kama na mume/mke nae ni mwanachama pia anapewa milioni tano inakuwa milioni 10.
π Kutoa mpaka milioni 15 pesa taslimu kwa siku kwenye ATM
Pia kutakuwa na akaunti za watoto ambao mtoto anakuwa na visa yaje
Mtoto mwenye akaunti ya Simba Executive Networks akifariki mzazi atapewa milioni mbili.