Tumepata pointi tatu za Coastal

Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani umemalizika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Freddy Michael Kouablan alitupatia bao la kwanza dakika ya 11 baada ya kuunganisha mpira wa kona uliopigwa na Clatous Chama.

Lucas Kikoti aliisawazishia Coastal dakika ya 25 baada ya kumalizia pasi ya mpira wa kona iliyopigwa na Modzaka.

Baada ya bao hilo tuliendelea kushambuliana kwa zamu huku kila timu ikitengeneza nafasi lakini hazikuweza kutumiwa.

Willy Onana alitupatia bao la pili dakika ya 72 baada ya kupokea pasi ya Chama na kabla ya kumpiga chenga mlinzi mmoja wa Coastal na kumchambua mlinda mlango Ray Matampi.

X1: Matampi, Miraji, Lawi, Shiga, Mulumba, Gwalala, Semfuko, Kikoti, Modzaka, Ajibu, Bekou

Walioonyeshwa kadi:Roland Bekou 63′

X1: Lakred, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Che Malone, Babacar (Mzamiru 58′), Miqussone (Kibu 58), Ngoma (Hamis 90+2), Freddy (Jobe 58′), Ntibazonkiza (Onana 67′), Chama

Walioonyeshwa kadi: Lakred 88′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER