Manula: Hatuna presha na mchezo dhidi ya ASEC

Mlinda mlango Aishi Manula amesema pamoja na ugumu na umuhimu wa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa Felix – Houphouet – Boigny lakini hatutaingia kwa presha.

Manula amesema mchezo huo ni mkubwa lakini hatutaogopa wala kuhofia bali tutafuata maelekezo ya walimu na lengo letu ni kuhakikisha tunashinda ugenini.

Manula ameongeza Simba ni timu kubwa na tumecheza mechi nyingi za aina hii katika mazingira tofauti kwahiyo tupo tayari kukabiliana na kila kitakachotokea.

“Tumeshakutana na aina hii ya mchezo, sisi kama wachezaji tupo tayari kufauata maelekezo tutakayopewa na walimu na lengo letu ni kushinda mchezo,” amesema Manula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER