Kauli ya Kocha Matola kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Tabora

Kocha Msaidizi Seleman Matola amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United utakaopigwa katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi saa 10 jioni.

Matola amesema tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani lakini tumejiandaa kuwakabili ili kupata pointi zote tatu.

Matola ameongeza kuwa kiungo mkabaji Fabrice Ngoma tayari amejiunga na wenzake hivyo benchi la ufundi litaamua kumtumia kama atakuwa yupo timamu kimwili.

“Tumefika salama mkoani Tabora, wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Tabora lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Matola.

Kwa upande wake mlinzi wa kati, Hussein Kazi amesema morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja yupo tayari kuhakikisha anapambana kuipigania timu.

Kazi amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuipa sapoti timu na hatimaye ushindi upatikane.

“Sisi wachezaji tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda,” amesema Kazi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER