Queens yafanya mazoezi ya mwisho Jamhuri

Timu yetu ya Simba Queens imefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Fountain Gate Princess.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi hao na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo huo.

Queens itaingia kwenye mchezo huo tukiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi mnono mabao 7-0 dhidi ya Alliance Girls tuliopata katika mechi iliyopita.

Morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja ameonyesha jitihada kubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa katika mchezo wa kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER