Kikosi kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Tembo FC utakaopigwa Jumatano saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex.
Wachezaji wote wameshiriki kikamilifu mazoezi hayo na hakuna ambaye amepata maumivu ambayo yametia hofu kukosekana katika mchezo huo.
Mazoezi hayo yamesmamiwa na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha