Serikali yatupongeza kwa kufuata maelekezo

Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limeipongeza Kamati ya Maboresho ya Katiba kwa kufuata maelekezo yote yaliyotakiwa kufanywa kabla ya mabadiliko ya katiba.

Pongezi hizo zimetolewa na Nicholaus Mihayo aliyekuwa akimuwakilisha Katibu Mkuu wa BMT katika Mkutano Mkuu wa Wanachama unaoendelea katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mihayo ameongeza kuwa Serikali inapenda kuona maelekezo inayotoa yanafuatwa yote kwa wakati na ndicho tulichokifanya.

“Tunaipongeza Simba kwa kufuata maelekezo na kuyafanyia kazi maboresho ya katiba. Hili ni jambo la mfano kwa timu nyingine. Serikali inawatakia kila la kheri,” amesema Mihayo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER