JESHI LA MNYAMA KAMILI KUIVAA LYON LEO

Kikosi chetu kimekamilisha maandalizi yote na sasa kiko tayari kuivaa Timu ya African Lyon katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), utakaopigwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Jana jioni timu ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye viwanja vyetu vya Mo Simba Arena huku wachezaji wote wakiwa kwenye hali nzuri tayari kwa mtanange huo ambao tunategemea utakuwa mgumu.

Kocha Mkuu, Didier Gomez Da Rosa amesema wachezaji wote wapo kamili na ameweka wazi anategemea kuwapa nafasi nyota ambao hawakucheza kwenye mchezo wa pili wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly Jumanne.

“Nategemea kuwapa nafasi wachezaji ambao walikosekana kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly, mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kufanya vizuri na kuingia hatua inayofuata,” amesema Kocha Da Rosa.

Baada ya mchezo wa leo kikosi kitacheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania siku ya Jumatatu kabla ya kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo wetu wa tatu wa Klabu Bingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Marrekh.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. MUNGU atujalie tuweze kushinda mechi ijayodhidiya jkt
    Ili wachezaji wetu wawe na molari kuka biliana na mechi za kimataifa
    MUNGU ibaliki SIMBA #NGUVU MOJA💪💪
    ❤❤❤🦁🦁🦁🦁🙏

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER