Kispika chatua Zanzibar kunogesha fainali ya Mapinduzi

Kikundi cha hamasa kutoka jijini Dar es Salaam chini ya King Faida kimewasili Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kunogesha fainali ya Kombe la Mapinduzi itakayofanyika usiku wa leo.

Baada ya kuwasili katika Bandari ya Zanzibar kikosi cha hamasa kiliingia mtaani na hapo walikutana na Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally na kuchukua ‘kispika’ na kuwahutubia Wazanzibar.

Akizungumzia na Wanasimba, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema tumetaka kuwaonyesha kuwa waliongia fainali ni Simba na ni timu kubwa ambayo inaweza kutamba kokote.

Ahmed ameongeza kuwa pamoja nakuwa mpira una matokeo ya kuumiza wakati mwingine lakini kwa jinsi tulivyojipanga ni dhahiri sisi ndio tutaibuka Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi.

“Hii ndio maana ya timu kubwa, kwanza tumeanza shamra shamra Bandarini na tukaenda hadi makao makuu ya Mlandege tutawachezesha mziki na wajue haikuwa bure usiku wa leo tunawafunga,” amesema Ahmed.

Ahmed amewaambia Wanasimba wote waliotoka Dar es Salaam wahakikishe wanakata tiketi ya boti ya saa tano kwakuwa sherehe za ubingwa zitaanzia hapo mpaka tutakapofika nyumbani.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER