Mawaziri Zanzibar watupongeza kwa kutangaza Utalii

Waziri wa Utamaduni Vijana na Michezo Zanzibar, Mh. Tabia Maulid Mwita ameupongeza Uongozi wa klabu kwa maamuzi ya kutangaza vivutio vya Utalii katika kipindi hiki cha michuano ya Mapinduzi inayoendelea Visiwani hapa.

Mh. Tabia ameyasema hayo baada ya kukabidhiwa zawadi ya jezi na Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally ikiwa ni muendelezo wa kutembelea Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili kufahamiana na kutangaza Utalii.

Mh. Tabia ameongeza kuwa maamuzi ya kutangaza vivutio vya Utalii ni mchango mkubwa tunafanya na hata kutembelea Viongozi wa Serikali nalo ni jambo zuri.

“Nawapongeza sana viongozi wa Simba kwa kuliona jambo hili na kulichukulia kwa umuhimu mkubwa mmefanya jambo zuri na nawapongeza,” amesema Mh. Tabia.

Kwa upande wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mh. Jamal Kassim Ally amesema jambo tunalofanya linatakiwa kuigwa na timu nyingine pamoja na Taasisi mbalimbali kutangaza Utalii wa nchi sababu unaongeza pato la taifa moja kwa moja.

“Nawapa hongera Simba kwa kutangaza Utalii wa Zanzibar, ni maamuzi mazuri ambayo yanafaida ya moja kwa moja kwa maendeleo ya nchi,” amesema Mh. Jamal.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER