Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex kuikabili Jamhuri katika mchezo robo fainali ya michuano ya Kombe Mapinduzi utakaopigwa kesho saa 2:15 usiku.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yanaweza kumfanya kuukosa mchezo wa kesho.
Morali za wachezaji zipo juu na tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na lengo la kuibuka na ushindi ili tutinge nusu fainali.
Tayari kocha msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi kuwa haitakuwa mechi rahisi na tunategemea kupata upinzani lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.