Timu yafanya mazoezi ya mwisho Gymkhana

Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Gymkhana kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca utakaoanza saa 10 jioni.

Wachezaji wote wameshiriki kikamilifu na morali ipo juu kuhakikisha tunashinda na kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali.

Ushindi katika mchezo wa kesho utakuwa ni wa kwanza kwenye hatua hii ndio maana tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa Wydad lakini tupo imara kupambana hadi mwisho ili kuwapa furaha Wanasimba na kubaki na alama tatu nyumbani.

Katika mchezo huo tutakosa huduma ya nyota wetu Saido Ntibazonkiza na Sadio Kanoute ambao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER