Miso Misondo kuongoza hamasa Mbagala Jumamosi

DJ Maarufu kwa sasa nchini, Hamisi Abdallah maarufu Miso Misondo ataongoza kikosi cha hamasa katika Uwanja wa Mbagala Zakhem siku ya Jumamosi kuelekea mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Wydad Casablanca.

Kama ilivyo kawaida kila mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika tukiwa nyumabani tunakuwa na hamasa kuzunguka jiji zima kwa ajili ya kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani na safari hii itaongozwa na Miso Misondo.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema lengo letu ni kuhakikisha mashabiki wanakuwa wengi uwanjani kwakuwa tunahitaji kupata ushindi.

“Jumamosi tunaanza hamasa katika Viwanja vya Zakhem kuelekea mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Wydad Casablanca na tutakuwa na DJ namba moja Tanzania kwa sasa Miso Misondo,” amesema Ahmed.

Kwa upande Miso Misondo amewataka wakazi wa Mbagala kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Zakhem kwa ajili ya kupata burudani pamoja na kununua tiketi.

“Wanasimba tukutane Mbagala Zakhem, tupo kwa ajili ya kuwapa burudani. Miso Misondo hatuna kazi ndogo,” amesema Misondo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER