Pamoja na kukiri ugumu kutokana na ubora wa Kagera Sugar kocha Mkuu Abdelhak Benchikha amesema tutaingia katika mchezo wa kesho kwa lengo la kutafuta pointi tatu.
Mchezo huo ambao utapigwa katika Uwanja wa Uhuru saa 10 jioni utakuwa mgumu lakini Benchikha amesema tunahitaji kupata ushindi.
Benchikha amesema ingawa hajawahi kuiona Kagera lakini ameifuatilia na amewaona jinsi wanavyocheza huku akikiri wapo vizuri.
Benchikha ameongeza kuwa kikosi kipo kwenye hali nzuri na wachezaji wapo kamili kuhakikisha tunapata ushindi ambao ndio lengo letu la kwanza.
“Utakuwa mchezo mgumu kesho, Kagera ni timu nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ingawa haitakuwa kazi rahisi,” amesema Benchikha.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinda mlango, Ally Salim amesema kwa upande wao wapo tayari kuhakisha wanapambana ili kupata pointi tatu kutoka kwa Kagera.
“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu, Kagera ni timu bora lakini tumejipanga kushinda,” amesema Ally.