Timu yetu ya Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Ilala Queens katika mchezo wa kirafiki iliyofanyika Uwanja wa Veterani uliopo Mbweni
Mshambuliaji Asha Rashid ‘Mwalala’ alitupatia bao ka kwanza baada ya kupokea krosi ya Mwanahamisi Omary.
Ilala Queens walisawazisha bao hilo kupitia kwa Rahma Sidedi dakika ya nane kwa shuti kali lilomshinda mlinda mlango wetu Gelwa Yona.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa upande mmoja zaidi Mwalala aliongeza bao jingine huku Shelda Boniface akifunga mawili na Zainabu Mohamed akifunga bao moja.
Mchezaji wa Ilala Thabita Salim alijifunga mwenyewe katika jitihada za kuokoa na kutupa ushindi huo mnono.
Queens ipo kwenye maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Princes utakaopigwa Disemba 9.