Novemba 25 kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaoanza saa 10 jioni.
Tumeweka hadharani viingilio vya mchezo huo,
Hivi hapa viingilio
Mzunguko – Tsh. 5,000.
VIP C – Tsh. 10,000.
VIP B – Tsh. 20,000.
VIP A – Tsh. 30,000
Platinum – Tsh. 150,000
Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia za mtandao.
Kuelekea mchezo huo tumekuja na Slogan ya “Twendeni Kinyama, Mashabiki Bomba” lengo ni kuonyesha kuthamini mchango wa mashabiki wetu.